Michezo

Top 5 ya Wachezaji ghali zaidi duniani 2017/2018

0

Vilabu vingi duniani huwekeza sana pia katika kufanya usajili bora, ili kuhakikisha kuwa wako na kikosi imara ambacho kitaisaidia klabu kufanya vizuri katika michuano watakayoshiriki. lli kuwa na kikosi bora lazima usajili wa gharama ufanyike.

Ifuatayo ni orodha ya wachezaji watano ambao ghali zaidi duniani:

1. Neymar Jr – Milioni £200 (Bilioni 609Tsh) – PSG

Neymar Jr Mchezaji bora

Neymar Jr.

Neymar Jr ni mshambuliaji, mwenye umri wa miaka 25 kutokea taifa la Brazil. Ni mchezaji ghali zaidi duniani ambapo uhamisho wake kutokea Klabu ya Barcelona kwenda PSG uligharimu kiasi cha paundi millioni £200 ambazo sawa na billioni 608Tsh.

2. Philippe Coutinho – Milioni £142 (Bilioni 435Tsh) – Barcelona

Philippe Coutinho Mchezaji bora

Philippe Coutinho

Philippe Coutinho ni KiungoMshambuliaji na Wingamwenyeumri wa miaka 25 kutokeataifa la Brazil. Ni mchezaji wa pili ghalizaididunianiambapouhamisho wake kutokeaklabu ya Liverpool kwenda Barcelona uligharimupaundimillioni £142 ambazo sawa na bilioni 435 zakitanzania.

Soma pia:  Jinsi ya Kupamba chumba cha kulala

3. Dembele – Milioni £97 (Bilioni 295Tsh) – Barcelona

Ousmane Dembele Mchezaji bora

Ousmane Dembele

Ousmane Dembele ni Mshambuliaji mwenye umri wa miaka 20 kutokea Ufaransa. Ni mchezaji wa tatu ghali zaidi duniani ambapo uhamisho wake kutokea Klabu ya Dortmund ya kwenda Barcelona uligharimu paundi milioni  £97 ambazo sawa na billioni 295 za kitanzania.

4. Pogba – Milioni £89 (Bilioni 270Tsh) – Manchester United

Paul Pogba Mchezaji bora

Paul Pogba

Paul Pogba ni Kiungo mwenye umri wa miaka 24 kutokea Ufaransa. Ni mchezaji wa nne ghali zaidi duniani ambapo uhamisho wake kutokea Klabu ya Juventus kwenda Manchester United uligharimu paundi milioni£89 ambazo sawa na bilioni 270 za kitanzania.

5. Bale – Milioni £86 (Bilioni 262Tsh) – Real Madrid

Gareth bale mchezaji bora

Gareth Bale

Gareth Bare ni Mshambuliaji mwenye umri wa miaka 28 kutokea Uingereza. Ni mchezaji wa tano ghali zaidi duniani ambapo uhamisho wake kutokea Klabu ya Tottenham Hostspur kwenda Real Madrid ulighanimu zaidi ya paundi milioni£86 ambazo sawa na bilioni 262 za kitanzania.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo