Makala

Jinsi ya Kupamba chumba cha kulala

0

Moja ya chumba pendwa huwa ni chumba cha kulala. Ndio maana wengi hupenda kuyaweka mandhari ya chumba katika muonekano wa kuvutia ama kuhamasisha kulala.

Hivyo kama unataka kunogesha chumba chako moja ya sehemu za kuanza nako ni kwenye meza ndogo inayokaa pembeni ya kitanda. Ndio sehemu unaiona ya kwanza unapoamka asubuhi na pia kabla ya kulala, hivyo unapaswa kuijali.

Kupamba chumba cha kulala

Chumba cha kulalia

Hizi ni dondoo chache za namna unavyoweza kupanga meza yako ya pembeni mwa kitanda, na kufanya chumba chako kivutie;

  • Tambua mtindo unaotaka kutumia kupamba meza yako ya pembeni; ukifahamu mtindo wako, itakusaidia kubuni ni muonekano wa namna gani unataka uwepo katika meza yako.
  • Ng’arisha kwa kuweka taa ya mezani; taa ya mezani ni moja yap ambo zuri la kuweka katika meza yako pembeni ya kitanda. Taa hiyo ina kazi nyingi mbali ya kupamba, lakini kama una tabia ya kuamka usiku, itakusaidia kukuangazia ili usije kujikwaa na kuanguka kwa kutoona.
  • Pamiliki kwa kuweka picha: uwekaji wa picha ni moja ya njia ya kupafanya paonekano ni sehemu yako binafsi. Unaweza kuweka picha zinazokukumbusha mambo mazuri ya familia. Unaweza pia kubadilisha na kuweka picha sanaa nzuri.
  • Weka trei ndogo: kwa ajili ya kuweka vitu vidogo vidogo pembeni ya kitanda chako. Trei ndogo ni timilifu kwa kutumia kupangia vitu kwenye meza ya pembeni mwa kitanda, ili kuepuka vitu kusambaa samba. Unaweza kuweka vitu vidogo vidogo kama herini, sarafu au vitu vingine vidogo.
  • Unaweza kuongeza nakshi kwa kuweka mmea pembeni ya kitanda kuongeza rangi; Kuweka mimea kwenye eneo lolote nyumbani huongeza uhai. Mimea kama ilivyo kwa taa ya mezani huongeza rangi na mvuto kwa muonekano mzima wa chumba. Kama wewe ni mtu usioweza kutunza mimea hai, basi weka mimea feki na hasa yakiwa ni maua.
  • Weka vipambo vidogo vizuri vya thamani; mapambo kama sanamu ndogo au saa vinaweza kufaa.
Soma pia:  Jinsi ya kupata Passport mpya ya Kielektroniki

Comments

Comments are closed.

More in Makala