Michezo

Hudson-Odoi kusaini miaka 5 Chelsea

0
Hudson-Odoi kusaini Chelsea
Callum Hudson-Odoi

Callum Hudson-Odoi anatarajia kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na Chelsea, kwa mujibu wa ESPN FC.

Mshambuliaji huyo kinda yupo kwenye mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake na ofa nne zilizotolewa na Klabu ya Bayern Munich zilikataliwa na sasa atabakia hapo Stamford Bridge.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England atasaini mkataba huo ambao utamfanya alipewa pauni 180,000 kwa wiki, huku kukiwa pia na uwezekano wa kuongezeka hadi pauni 200,000 kwa wiki.

Ofa ya mwisho ya Bayern kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 ilitolewa Januari mwaka huu ya pauni milioni 35.

Hudson-Odoi amekubali kusaini mkataba mpya baada ya kushawishiwa na kocha wa sasa, Frank Lampard ambaye amemwambia kwamba yupo kwenye mipango yake ya baadae.

Soma pia:  Eden Hazard ni Mlevi wa Filamu

Kocha wa zamani wa Chelsea, Maurizio Sarri alikuwa hampi nafasi ya kucheza Hudson-Odoi na hivyo kuibua uvumi kwamba mchezaji huyo angeondoka kipindi hiki cha majira ya joto.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo