Michezo

Real Madrid wakomaa na Pogba

0
Real Madrid wakomaa na Pogba
Paul Pogba

Klabu ya Real Madrid wapo tayari kutoa kiasi cha pauni milioni 150 kwa ajili ya kumsajili Paul Pogba na pia wapo tayari kumpa mshahara wa pauni 600,000 kwa wiki.

Mchezaji huyo wa Manchester United amekuwa katika rada ya Real Madrid ambayo kwa sasa ipo chini ya kocha, Zinedine Zidane kwa muda mrefu na imefahamika kuwa mkakati wa kumnasa nyota huyo ni kama unakwenda sawa kwa sasa.

Tatizo lililopo ni kwamba Real hawawezi kulipa mishahara miwili kwa Gareth Bale na Pogba kwa wakati mmoja, hivyo ni lazima wamuuze nyota wa Wales ndipo wamnase Bale.

Msimu huu Zidane, ameshawanunua wachezaji watano katika dirisha la usajili linaloendelea na amemfanya Pogba kuwa namba moja katika jitihada za usajili.

Soma pia:  Benzema Afunga bao la 400 LaLiga

Katika siku za karibuni kulikuwa na habari kwamba Pogba amekalishwa chini na viongozi wa Manchester United na kumtuliza lakini taarifa kutoka kambini kwake zinasema kuwa mchezaji huyo bado ana mpango wa kutua Hispania.

Katika hatua nyingine, Bale, yuko katika kikosi cha Real huko Amerika Kaskazini kwa ajili ya mechi za kujiandaa na msimu na habari mbaya ni kwamba haelewani na kocha wake Zidane.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo