Makala

Top 10 ya Nchi tajiri Afrika kwa GDP

0

Bara la Afrika ni Bara la pili kwa ukubwa duniani, ambapo lina jumla ya  nchi 54 na wakaazi zaidi ya bilioni 1.216. Kutokana na takwimu za mwaka 2012, Uchumi wa Barani Afrika unategemea Sekta ya Biashara, Kilimo, Nguvu Kazi na Viwanda.

Ingawa Bara la Afrika limebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi lakini asilimia kubwa ya wananchi ni masikini na wamekuwa wakitumika kwa miaka mingi. Inatarajiwa ifikapo mwaka 2050 uchumi wa Barani Afrika utafikia dola trillioni 29 zakimarekani.

TOP 10 ya Nchi tajiri Afrika kwa kuzingatia Takwimu za mwaka 2017 ni kama ifuatavyo;

10. Namibia – $11,800 (Tsh 26,550,000)

Nchi tajiri Afrika

Windhoek, Mji mkuu wa Namibia

Namibia ipo Kusini mwa Bara la Africa na ina idadi ya watu takriban millioni 2.5.

Kwa mujibu wa Takwimu za mwaka 2017 zinaonyosha kuwa GDP ya pato kwa kichwa ni dola $11,800 sawa na (Tsh 26,550,000), na imekuwa ni nchi ya kumi tajiri zaidi barani Africa.

Ambapo sekta ya Madini, Kilimo, Uzalishaji na Utalii ndio zimechangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa taifa hilo.

Hata hvyo gharama za maisha nchini Namibia zipo juu kutokana bidhaa nyingi zinazotumika nchini humo zinatoka nje ya nchi. Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Namibia pia kipo juu, karibia asilimia 27.4%.

9. Misri – $12,100 (Tsh 27,000,000)

Nchi tajiri Afrika

Cairo, Mji mkuu wa Misri

Misri ipo Kaskazini mwa Afrika, imepakana na nchi tofauti ambazo ni Israili, Sudani, Libya, n.k.

Ni nchi ya tisa barani Afrika kwa utajiri ambapo GDP yake ya pato kwa kichwa ni dola $12,100 sawa na (Tsh 27,000,000).

Soma pia:  Vituo vya TV vimefungiwa baada ya kurusha Raila akila kiapo

Uchumi wa Misri unategemewa na Kilimo, Utalii, Gesi Asilia, Petroli na shughuli zingine za kuichumi.

Pia asilimia kubwa ya raia wa misri hufanya kazi nchi za nje ambapo malipo ya wafanyakazi hao vilevile huchangia utajiri wa taifa hilo.

8. Africa Kusini – $13,500 (Tsh 30,375,000)

Nchi tajiri Afrika

Cape Town, Afrika Kusini

Africa Kusini ni nchi ambayo ipo kusini mwa Bara la Afrika na imepakana na Namibia, Bostwana, Swaziland, Lesotho na Msumbiji.

Ni nchi ambayo GDP yake iko juu zaidi kulinganisha nchi zingine za Afrika lakini pia inakumbwa idadi kubwa ya watu wasio na ajira, Umasikini pamoja na kuwa na pengo kubwa kati ya masikini na tajiri.

Hata hivyo Afrika Kusini imechukuwa nafasi ya nane kwa utajiri Barani Afrika kulingana na takwimu za mwaka 2017 ambapo GDP ya pato kwa kichwa ni dola $13,500 sawa na (Tsh 30,375,000).

7. Libya – $14,200 (Tsh 31,950,000)

Nchi tajiri Afrika

Tripoli, Mji mkuu wa Libya

Libya ipo Kaskazini mwa Bara la Afrika na ni nchi ya nne kwa ukubwa zaidi Barani humo.

Ina jumla ya watu millioni 6 na GDP ya pato kwa kichwa ni dola $14,200 sawa na (Tsh 31,950,000).

Ni nchi iliyobarikiwa na hifadhi kubwa ya mafuta. Imeshika nafasi ya saba kwa Utajiri zaidi Barani Afrika.

Uchumi wake unategemea zaidi mafuta lakini vilevile imebarikiwa kuwa na wa Gesi Asilia na gypsum.

Hata hivyo licha ya Utajiri wote huo, idadi ya watu wasio na ajira ni kubwa na kufikia kiwango cha takriban 21%. Pia Libya inakumbwa na machafuko ya kiasiasa ambapo hudhoufisha uchumi wa taifa hilo na kusababisha kurudi nyuma kwa maendeleo.

Soma pia:  Top 5 ya Wachezaji ghali zaidi duniani 2017/2018

6. Algeria – $15,000 (Tsh 33,750,000)

Nchi tajiri Afrika

Tripoli, Mji mkuu wa Libya

Algeria ipo Kaskazini mwa Afrika na vilevile ni nchi kubwa yao Barani Afrika. Ina idadi ya watu millioni 40.

Ni nchi ya sita kwa utajiri Barani Afrika ambapo GDP ya pato kwa kichwa dola $15,000 sawa na (Tsh 33,750,000).

Uchumi wa Algeria unategemea petroli na Gesi Asilia.

5. Botswana – $16,900 (Tsh 38,025,000)

Nchi tajiri Afrika

Gaborone, Bostwana

Bostwana ipo Kusini mwa Bara la Afrika. Nchi hii inasifika kuwa na demokrasia imara na idadi ya watu ni kwenye millioni 2.1. Bostwana ni nchi ya tano tajiri Barani Afrika.

Uchumi wa Bostwana unakuwa kwa hara sana na inachukuliwa kuwa ni nchi ya kipato cha kati na pia ni nchi yenye mfumo wa kisasa wa benki na kiwango cha chini cha madeni ya kigeni.

Uchumi wake unategemea Madini. Bostwana imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi kama vile uranium, dhahabu, almasi, shaba n.k.

4. Gabon – $19,300 (Tsh 43,425,000)

Nchi tajiri Afrika

Libreville, Gabon

Gabon ni nchi ya Afrika ya Kati iliopo katika pwani ya Afrika Magharibi. Gabon imepakana na Guinea ya Equatorial, Cameroon na Jamhuri ya Kongo.

Ni nchi ya nne kwa utajiri Barani Afrika ambapo GDP ya pato kwa kichwa dola $19,300 sawa na (Tshs 43,425,000).

Uchumi wa Gabon unategemea mafuta, hata hvyo, kwa miaka ya karibuni, uzalishaji wa mafuta nchini Gabon umeshuka na baadhi ya wataalamu wanatabiri kuwa utaisha.

Soma pia:  Winnie Mandela Kuzikwa leo

Gabon imeshika nafasi ya nne kutokana na serekali kumiliki kiwango kikubwa cha pesa na idadi ya watu ni ndogo, hata hivyo inaripotiwa kuwa wakaazi wengi ambao ni masikini.

3. Mauritius – $20,500 (Tsh 46,125,000)

Nchi tajiri Afrika

boardwalk, Mauritius

Mauritius kisiwa ambacho kimezungukwa na bahari ya hindi. Imepata Uhuru mwaka 1968 na ina idadi ya watu millioni 1.3.

Ni nchi ya tatu tajiri Barani Afrika.

Uchumi wa Mauritius unategemea Sekta ya Utalii zaidi ingawa pia kilimo inachangia kukuwa kwa uchumi wa taifa hilo.

Nchi ya Mauritius inasifika kuwa na fukwe nzuri za bahari pamoja na hali ya hewa nzuri.

2. Seychelles – $28,000 (Tsh 63,000,000)

Nchi tajiri Afrika

Victoria, Mji Mkuu wa Seychelles (Visiwa vya Shelisheli)

Seychelles imezungukwa na Bahari ya Hindi, Imeundwa na visiwa vidogo 115.

Ina idadi ya wakaai 92,000, na ndio nchi yenye idadi ndogo ya watu barani Afrika.

Ni nchi ya pili kwa Utajiri Barani Afrika ambapo GDP ya pato kwa kichwa dola $28,000 sawa na (Tsh 63,000,000).

Seychelles inajulikana kuwa ni nchi yenye maendeleo zaidi barani Afrika.

Uchumi wake unategemea zaidi Utalii kwa kiasi kikubwa na vilevile uvuvi unachangia uchumi wa taifa hilo.

1.Equatorial Guinea – $38,700 (Tsh 87,075,000)

Nchi tajiri Afrika

Bata, Equitorial Guinea

Equatorial Guinea ni nchi ipo Afrika ya Kati, ni nchi ndogo sana. Ina idadi ya watu millioni 1.2.

Nchi hii imekuwa ni ya kwanza tajiri barani Afrika kutokana na kuwa na idadi ndogo ya watu.

Hata hivyo ingawa ina GDP kubwa lakini imeripotiwa kuwa ina wakaazi wengi wa hali ya chini ambao wanakosa haki za msingi kama vile maji safi na salama.

Comments

Comments are closed.

More in Makala