Michezo

Ronaldo afutiwa Shtaka la Ubakaji Marekani

0
Ronaldo afutiwa Shtaka la Ubakaji
Ronaldo akiwa na Kathryn Mayorga

Nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo, hatakabiliwa na shtaka lolote baada ya kutuhumiwa na madai ya unyanyasaji wa kingono, waendesha mashtaka wa Marekani wamesema.

Mwanamke mmoja, Kathryn Mayorga mwenye umri wa miaka 34, alidai kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid alimbaka katika hoteli moja mjini Las Vegas mwaka 2009.

Iliripotiwa kuwa Kathryn alikubaliana na nyota huyo kusuluhisha kesi hiyo kimya kimya nje ya mahakama mwaka 2010.  Lakini aliamua kufungua tena kesi hiyo mwaka 2018, baada ya Ronaldo kupinga madai hayo.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, waendesha mashtaka wa mjini Las Vegas walisema madai hayo hayakuweza kuthibitishwa.

“Hakuna shtaka litakalotolewa,” taarifa hiyo ilisema. Gazeti la kila wiki la Ujerumani Der Spiegel, lilichapisha taarifa kuhusu madai hayo mwaka jana.

Soma pia:  Mbunge mbaroni kwa Ubakaji

Gazeti hilo liliandika kuwa Kathryn, alitoa ripoti katika kituo cha polisi cha Las Vegas muda mfupi baada ya tukio hilo.

Ubakaji Ronaldo Marekani

Ronaldo akiwa na Kathryn Mayorga

Comments

Comments are closed.

More in Michezo