Burudani

Nyoshi atoa somo bendi za dansi

0
Nyoshi bendi za dansi
Nyoshi El Sadaat

Rais wa bendi ya muziki wa dansi inayokuja kwa kasi ya Bogos, Nyoshi El Sadaat amezitaka bendi zisikate tamaa na badala yake zikaze buti, kwa madai kwamba soko bado limebana.

“Kukata tamaa ni kukubali kushindwa, hivyo jambo la msingi ni kukaza buti na kuendelea kukomaa, kwani ipo siku muziki wa dansi utarudi kwenye levo kama zamani,” alisema Nyoshi.

Nyoshi ambaye bendi yake hiyo inaundwa na sehemu kubwa ya wanamuziki vijana, aliliambia gazeti hili jana kuwa kikosi chake kiko imara na kinaendelea kutoa burudani kama kawaida bila kuyumba.

Alisema, siri ya mafanikio ni kupambana, hivyo anawashauri wanamuziki wa bendi nyingine kuzingatia hilo ili waendelee kutoa burudani lakini pia wakitunga nyimbo ambazo zinaweza kurudisha bendi zao kwenye soko.

Soma pia:  Nyoshi aeleza sababu za kukosa mapato

“Katika mafanikio hakuna njia ya mkato, tuendelee kukomaa tu ipo siku kitaeleweka na tutafanya maonyesho makubwa kama zamani, ila tukumbuke kuwa hakuna mafanikio yasiyo na changamoyo,” alisema.

Alisema, kwa sasa ni kama muziki wa dansi umelala, kwa madai kwamba baadhi ya bendi hazifanyi kazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kukosa mashabiki hali ambayo inaonyesha kuwa mambo siyo mazuri.

Comments

Comments are closed.

More in Burudani