Burudani

Benpol amvisha pete mchumba wake Arnelisa

0

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Benpol jana alimvisha pete ya uchumba mchumba wake Arnelisa ikiwa ni ishara ya kuelekea kufunga pingu za maisha kwa wapendwa hao wawili.

Benpol amvisha pete mchumba wake
Benpol na Arnelisa

Benpol amethibitisha hatua hiyo muhimu kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuweka picha na mpenzi wake akionekana anamvalisha pete ya uchumba.

Alisema kwamba hatua hiyo muhimu itafanikisha maisha bora ya familia yao ambayo malengo yake ni mafanikio ya kimaisha.

“Tumuombe Mungu yasije kutokea kama ya wengine ambao wao huishia kuvalishana pete ila ndoa hubaki kitandawili,” alisema Ben pol.

Soma pia:  Raila Odinga Kujiapisha rasmi Leo

Comments

Comments are closed.

More in Burudani