Burudani

Nyoshi aeleza sababu za kukosa mapato

0
Nyoshi aeleza sababu za kukosa mapato
Nyoshi Sadat

Mwanamuziki wa muziki wa dansi, Nyosh Al Sadat amesema kinachowafanya wakose mapato katika matamasha wanayofanya ni muda mchache wa kufanya matamasha katika kumbi za muziki.

Akizungumzia juu ya changamoto ya muda katika kumbi za muziki, anasema inapofika saa 5 usiku wateja wengi ndiyo wanaingia kwenye kumbi, lakini ikifika saa 6 inabidi wafunge kufuata amri ya polisi.

Alisema hata Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam alipotoa agizo la kumbi hizo kufungwa saa 8 usiku alipokuwa kwenye sherehe za kuadhimisha siku ya kuzaliwa mwanamuziki Nassib Abdul ‘Diamond’, polisi walisema kuwa hilo sio tamko rasmi.

“Wateja wanashindwa kupata huduma za muziki sababu muda ambao sisi tunafunga, ndio muda ambao wateja hutoka majumbani,” alisema. Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda alisema anatarajia kulifanya jiji la Dar es Salaam liwe linapiga muziki saa 24.

Soma pia:  Nyoshi atoa somo bendi za dansi

Comments

Comments are closed.

More in Burudani