Burudani

Abdu Kiba atamani alipo kaka yake Ali Kiba

0
Abdu Kiba atamani alipo kaka yake Ali Kiba
Abdu kiba akiwa na kaka yake

Msanii wa muziki wa Bongofleva, Abdu Kiba amesema anatamani kufi kia hatua nzuri ya kimuziki kama aliyofi kia kaka yake Ali Kiba ambaye pia ni msanii.

Abdu Kiba alisema ana imani kutokana na kujituma kwake kuna wakati utafika hatua nzuri kama aliyofika kaka yake.

Alisema hakuna kinachoshindikana katika ulimwengu na tayari ameanza kuandaa mikakati ya kuhakikisha anafikia mafanikio yanayofanana na Ali Kiba.

“Chini ya jua hakuna kinachoshindikana ajuaye siri ni Mungu, ila wote tuna imani tufike walipofika wasanii wengine kama alivyofika kaka yangu Ali Kiba,” alisema Abdu Kiba.

Alisema itakuwa kama ni miujiza na wengi hataamini na kuongeza njia bocfika hatua hiyo ni kutoa kazi zenye ubora wa kiwango cha juu na zenye kukubalika

Soma pia:  Dogo Janja atangaza rasmi kuachana na Uwoya

Comments

Comments are closed.

More in Burudani