Burudani

Msafiri Zawose kumalizia ziara yake Uholanzi

0
Msafiri Zawose kumalizia Uholanzi
Msafiri Zawose

Baada ya kufanya kweli katika nchi za Denmark, Sweden, Belgium msanii Msafiri Zawose leo anamalizia sanaa yake ya muziki wa asili nchini Uholanzi katika ukumbi wa Paradiso baada ya jana kurindima kwenye ukumbi wa Podium Grounds nchini humo.

Akizungumza kutoka Uholanzi, Zawose alisema muelekeo ni mzuri na unazidi kuleta matumaini ya kazi yake kwani umezaa matunda kwa kukusanya idadi kubwa ya mashabiki katika nchi alizofanya maonesho yake.

“Huku nimewaletea electronic organic music, nyimbo 13 mpya, nimeambatana na Dj set nzima kutoka Marekani ambayo sio ya mchezo,” alisema Zawose.

Zawose alisema shoo zake yuko na timu nzima ya watu watano watatu wanamuziki, meneja wa tour na dereva ambaye wamezunguka naye nchi zote kwa gari maalum.

Aidha Zawose aliweka bayana nyimbo ambazo amewapelekea mashabiki wa muziki wa Ulaya ni pamoja na Nzala Urugu, Polepole, Chib-itenyi, Nosaga, Kunyemo, Mbeleko, Tamaduni, Tusife Majanga, Mazingira, Mdara, Mashariki ya mbali, Malugaro na Hali halisi.

Msafiri Zawose ziara Uholanzi
Msafiri Zawose
Msafiri Zawose Ulaya
Msafiri Zawose

Comments

Comments are closed.

More in Burudani