Burudani

Wema Sepetu aibuka na Tuzo mbili

0
Wema Sepetu aibuka na Tuzo mbili
Wema Sepetu

Nyota wa Filamu za bongo movie ambaye aliyewahi kuwa miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu aibuka na tuzo mbili ambazo juzi kwenye hafla ya tuzo za wasanii wa filamu zilizofanyika Dar es Salaam.

Tuzo hizo zilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, ambapo zilihidhuriwa na mashabiki na wadau wa filamu nchini.

Nyota huyo alipata tuzo mbili kwenye hafla hiyo katika kipengele cha mwigizaji bora kupitia filamu yake ‘Heaven Sent’ na mwigizaji bora wa mwaka wa kike.

Akizungumza mara baada ya kupewa tuzo hizo, Wema alisema kwamba amefurahi kitendo cha kupata tuzo kwani mchango wake unaonekana kwa jamii.

Alisema kwamba anamkumbuka marehemu Steven Kanumba kwani yeye ndio aliyeona kipaji chake tangu awali. Pia alisema kuwa anawashukuru waandaaji wa tuzo hizo na kwamba zimemtegenezea heshima kwa jamii kwa kupitia kazi yake ya sanaa ya filamu.

Soma pia:  Miss Tanzania Kuanza kusakwa leo

“Nimefurahi kupata tuzo hizi kwani inaonyesha ni kiasi gani nina mchango kwa jamii, hivyo ikiwa ni pamoja na kuibua vipaji zaidi,” Alisema Wema.

Wema Sepetu aliongezea kwa kusema; “Kwa kiasi kikubwa ninamkumbuka marehemu Kanumba kwani ni mmoja ya wasanii ambao walitambua kipaji changu awali”.

Wema Sepetu alisema kwamba lengo lake ni kuhakikisha anaendelea kufanya vizuri ili kuendeleza kipaji alicho nacho ikiwa ni pamoja na kuburudisha jamii.

Wema Sepetu
Wema Sepetu

Comments

Comments are closed.

More in Burudani