Top Stories

Wanafunzi kupatiwa maziwa shuleni Rwanda

0
Wanafunzi kupatiwa maziwa shuleni Rwanda
Wanafunzi Rwanda

Wizara ya Elimu imetangaza mkakati wa kuhakikisha kila mwanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini hapa, wanapata angalau nusu lita ya maziwa kwa siku katika chakula wanachopatiwa shuleni.

Kutokana na mkakati huo, wanafunzi watatumia takribani lita 180 za maziwa kwa mwaka ili kuwaepusha na matatizo ya magonjwa ya utapiamlo na kula lishe kamili ambao mwili unahitaji.

Waziri wa Elimu, Eugene Mutimura alitaka shule kuanza kutekeleza mkakati kabla ya wiki ijayo kwani kuna aina mbili za wanafunzi wanaopata vyakula shuleni na wasiopata na serikali inachangia faranga 56 kwa kila mwanafunzi kwa ajili ya chakula.

Alisema kwa kawaida chakula kwa wanafunzi hupikwa kwa hutumia unga, maharage na vyakula kama hivyo katika programu za shule wanatakiwa kuweka maziwa.

Soma pia:  Historia ya Intaneti, Mambo 16 huenda ulikuwa huyajui kuhusu Intaneti

Katika kuhakikisha suala hilo linafanikiwa, wizara watafanya kazi na shule, Wizara ya Serikali za Mitaa na Kilimo na wadau wengine, huku maziwa yakipatikana katika vituo vya kukusanyia maziwa kwa faranga 200 na faranga 300 kwa lita

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories