Makala

Historia ya Intaneti, Mambo 16 huenda ulikuwa huyajui kuhusu Intaneti

0

Kadiri miaka inavyozidi kwenda, idadi kubwa ya watu inazidi kutumia huduma mbalimbali za intaneti kwa namna tofauti tofauti lakini ulishawahi kujiuliza maana halisi ya msamiati huu?

Maana ya Intaneti inaweza kufafanuliwa kuwa ni mfumo wa kudunia wa muunganiko wa mtandao wa kompyuta unaotumia teknolojia ya TCP/IP ili kuwafikia mabilioni ya watu kote duniani.

Historia ya Intaneti

Intaneti

Asili ya teknolojia hiyo, historia inasema kuwa ni nchini Marekani ambako ilitumiwa na idara ya ulinzi nchini humo, ili kuwaunganisha wanasayansi na watalaamu wakubwa kutoka vyuo vikuu mbalimbali duniani.

Miaka mingi iliyopita, wataalamu wa mawasiliano ya kidijitali waliwahi kuelezea intaneti kuwa ni mtandao wa mitandao, ambao leo hii unatumika kama njia kuu ya mawasiliano ya kisasa kuanzia yale binafsi, kiserikali na kibiashara.

Kwa jinsi ulivyoundwa, mtandao wa intaneti haumilikiwi na mtu yeyote na hauna mamlaka ya kiserikali yenye uwezo wa kusema ndiye mmiliki halali kwa asilimia 100 na sababu kuu ya kufanya uwe hivyo ni ili kuwe na usalama hasa nyakati za vita na matukio ya kigaidi.

Jambo ambalo ninalitamani kulizungumzia kwenye makala hii, ni kuondoa asumba iliyopo miongoni mwa watu kuwa intaneti na kitu kinachoitwa ‘World Wide Web’ yaani ‘WWW’ ni kitu kimoja kikiwa na majukumu sawa, hili si kweli.

Intaneti ni eneo kubwa la miundombinu inayowezekana kuguswa na ile isiyowezekana kuguswa ‘hadware and software’ ambayo inaruhusu muingiliano wa kompyuta mbalimbali.

WWW kwa upande wake, ni sehemu kubwa ya kutunza data za kikompyuta, ambayo inahusisha makusanyo mengi ya nyaraka na rasilimali zingine zinazounganishwa na ‘hyperlinks’.

Kwa maelezo mafupi, WWW ni uwanja unaoruhusu mtumiaji wa kompyuta kujivinjari kwenye intaneti kwa kutumia vivinjari ‘browsers’ kama vile Google chrome au Mozilla Firefox.

Soma pia:  Mradi wa Pasipoti ya Kielektroniki pamoja Faida zake

Historia ya intaneti inaanzia miaka ya 1950 ikienda sambasamba na maendeleo ya ugunduzi wa kompyuta za kisasa zenye muonekano mbalimbali na uwezo tofauti tofauti kulingana na matumizi.

Ni wazi kuwa, ulimwengu wa intaneti wa leo ulianzishwa na mwanasayansi wa kompyuta wa Uingereza Tim Berners Lee.

Ugunduzi wa Tim kwenye kuunda intaneti yake ya kwanza, moja kwa moja kubadili ulimwengu, vyombo vya habari, mahusiano, burudani na mambo mengine mengi.

Intaneti ya leo, ni dhahiri kuwa tunaona mambo mengi ambayo intaneti imepitia tokea kuanzishwa kwake hadi hivi leo.

Teknolojia hii iliyorahisisha dunia ya utandawazi, ina mambo mengi ambayo kati ya hayo leo ninakujumuishia kama ifuatavyo:

1) Tovuti ya kwanza kuundwa bado ipo na inafanya kazi hadi leo. Jambo pekee ni kuwa tovuti hiyo inaonekana vile vile kama ilivyokuwa zamani na unaweza kuina kwa kutembelea http://info.cern.ch/hypertext/WWW/TheProject.html

2) Kwenye utafiti uliofanywa na kampuni ya Radicati, takriban barua pepe bilioni 247 hutumwa kwa siku kupitia tovuti tatu kuu za barua pepe ikiwemo Yahoo, Gmail na Hotmail. Radicati inakadiria kuwa takriban barua pepe 247 hutumwa kila siku. Inaelezwa kuwa asilimia 90 ya barua pepe hizi ni barua pepe hatarishi (SPAM) na Virusi, hivyo kuwa makini na barua pepe unazofungua.

3) Tweet ya kwanza ilichapishwa Machi 21 mwaka 2006 na Jack Dorsey. Nani alifahamu kuwa Twitter ingekuwa maarufu duniani kama ilivyo leo? Machi 21 mwaka huo, Jack Dorkey aliandika tweet ya kwanza iliyokuwa inasema, “just setting up my twttr.” lakini hivi leo Twitter imeshakuwa na mamilioni ya watumiaji ulimwenguni kote.

Soma pia:  Mambo 10 huenda ulikuwa huyafahamu kuhusu Ronaldo

4) Video iliyotazamwa kuliko zote kwenye mtandao ni Despacito, Wimbo wa Despacito ulioimbwa na Luis Fonsi na Daddy Yankee ni wimbo unaoongoza kwa kutazamwa na watu wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube. Wimbo huu umeshatazamwa mara bilioni 6.17 hadi sasa.

5) Mgunduzi wa intaneti Tim Berners-Lee alipewa cheo cha Knight na Malkia Elizabeth wa Uingereza. Kutokana na ugunduzi mkubwa alioufanya, Tim Berners-Lee, malkia wa Uingereza alimpa cheo hicho cha heshima cha Knight kwenye serikali yake mwaka 2003.

6) Saa 300 za video hupakiwa kila dakika kwenye mtandao wa YouTube ambao ni mtandao maarufu wa kusambaza video mtandaoni. Tovuti hii hupokea video kutoka kwa watumiaji mbalimbali duniani kote.

7) Neno kuperuzi mtandaoni (surfing the internet) liliundwa mwaka 1992. Kabla ya mwaka 1992 neno (Surfing the internet), halikuwa linafahamika hadi pale Jean Polly alipoandika makala iliyosomwa sana na kupakuliwa na watu wengi na kusababisha kusambaa kwa neno hili.

8) Mitandao ya kutafuta wapenzi (Dating sites), inazalisha takriban dola bilioni 2.2 kila mwaka hii ni kutokana na teknolojia kubadilisha mfumo wa maisha. Watu hutafuta wapenzi au wenzi wa maisha kwenye mtandao. Hili limesababisha tovuti za kutafuta wapenzi kuzalisha zaidi ya bilioni 2.2 kwa mwaka 2014 pekee.

9) Asilimia 10 ya wahalifu wa kijinsia wanatumia mitandao ya kutafuta wapenzi kutokana na umbali au kutofahamiana vyema, wahalifu wengi wa kijinsia hutumia mitandao ya kutafuta wapenzi kufanya uhalifu wao.

10) Takriban watoto milioni moja wamezaliwa kutokana na watu waliokutana kupitia mtandao wa match.com. Mtandao huo wa match.com unadai kuwa takriban watoto milioni moja wamezaliwa kutokana na watu waliokutana kwenye tovuti hiyo ya kutafuta wapenzi.

Soma pia:  Fahamu namna ya kukabili moto wa jikoni

11) China ina kambi za kutibu waathirika wa kutawaliwa na mtandao (internet addict). Wakati China ikiwa na watumiaji wa intaneti wapatao zaidi ya milioni 721, inaaminika kati yao 23 ni waathirika wa kutawaliwa na mtandao. Hivyo wameanzisha kambi mbalimbali za kuwasaidia watu hao.

12) Watumiaji wengi wa intaneti ni roboti na programu haribifu (malware). Wakati mwingine unaweza kufikiri watumiaji wa mtandao ni watu pekee. Lakini asilimia kubwa ni roboti na programu haribifu zilizobuniwa na watu mbalimbali ili kutimiza shughuli fulani.

13) Tweets milioni 500 zinatumwa kila siku kutokana na Twitter kuwa na watumiaji milioni kadhaa, inaaminika kuwa zaidi ya tweets milioni 500 hutumwa kila siku.

14) Wewe huwa unatumia kisehemu kidogo tu cha mtandao. Ni wazi kuwa sehemu unayotumia kwenye intaneti ni sehemu ndogi sana ambayo inaonekana kwenye injini pekuzi (search engines). Ipo sehemu nyingine ambayo imefichwa kwenye injini pekuzi (dark web); sehemu hii inajumuisha taarifa binafsi za watu, taasisi na makampuni mbalimbali. Unaweza kuperuzi sehemu iliyofichwa ya intaneti kwa kutumia kivinjari (browser) ya Tor.

15) Tovuti 30,000 zinadukuliwa kila siku, kutokana na kuongezeka kwa uhalifu wa kwenye mtandao, inakadiriwa kuwa zaidi ya tovuti 30,000 hudukuliwa na wadukuzi kila siku.

16) Suala la mwisho ninalotaka kukushirikisha leo kuhusu intaneti ni IMDb, kwamba ilikuwepo tangu miaka ya 1990. Tovuti hii maarufu ya kutafuta video, filamu, vipindi vya televisheni pamoja na michezo ya video, ilianzishwa Oktoba 21, mwaka 1990 na mtu anayeitwa Col Needham, ambaye tangu wakati huo IMDb imedumu hadi leo.

Comments

Comments are closed.

More in Makala