Top Stories

Putin na Macron wasimamia amani Syria

0
Putin na Macron
Putin na Macron

Rais wa Urusi, Vladimir Putin na rais mwenzake wa Ufaransa, Emmanuel Macron, wamekubaliana katika kuratibu mpango wa kurejeshwa kwa amani nchini Syria.

Ikulu ya Urusi ilisema kuwa viongozi hao wawili walifikia makubaliano hayo juzi katika mazungumzo yao yaliyofanyika kwa njia ya simu.

“Pande hizi mbili zilibainisha haja ya kukuza mazungumzo ya kisiasa ya Syria pamoja na kuzindua kazi ya Kamati ya Katiba mapema iwezekanavyo,” ilisema taarifa ya Ikulu ya Urusi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ikulu ya Urusi, Putin na Macron walijadiliana kuhusu eneo la kaskazini-mashariki mwa Syria pamoja na Idlib, huku Putin akionya kuhusu wanamgambo nchini humo kutayarisha silaha za kemikali.

Imeelezwa kuwa marais hao wawili kwa pamoja, walikubaliana kutekeleza azma yao ya kutaka kuirudisha Syria katika hali ya amani.

Soma pia:  UN yasaidia Sudan Kusini kujikinga na ebola

Viongozi hao pia walikubaliana kushirikiana katika kutatua mgogoro wa ndani nchini Ukraine pamoja na mfumo wa kundi la Normandy linalohusika na utatuzi wa vita mashariki mwa Ukraine.

Kundi hilo linalojumuisha nchini za Ujerumani, Urusi, Ukraine na Ufaransa. Katika hatua nyingine, Putin pamoja na washirika wake ambao ni Uturuki na Iran walikubaliana pia katika mambo kadhaa kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Syria ikiwemo kusukuma juhudi za kufanyika kwa mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo.

Putin alisema kuwa wengi wa washiriki katika kamati ya katiba ikiwemo Serikali ya Syria na upinzani wamekubaliana katika mambo mbalimbali, hivyo hatua inayofuata ni ufafanuzi wa vipengele vya kisheria kwa ajili ya utendaji wake.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories