Burudani

Vee Money awakubali waandaaji wa Bongo

0
Vee Money awakubali waandaaji wa Bongo
Vee Money

Msanii wa kizazi kipya,Vanessa Mdee ‘Vee Money’ anayetamba na Albamu ya ‘Money Monday’, amesema hategemei kufanya kazi na waandaji wa video za kutoka nje, kwani wandani wamejitambua na wanafanya kazi nzuri.

Akipiga Stori na Showbiz Xtra, Vee Money ambaye ametambulisha pia video yake ya wimbo unaopatikana kwenye Albamu yake hiyo uitwao ‘Wet’ aliomshirikisha G Nako, aliongeza kwamba hata akiwa na hamu ya kufanya kazi na mwandaji wa nje, atahakikisha anamleta Bongo ili ashirikiane na waandaji wa ndani kufanya kazi.

“Kwa sasa kiukweli tutabanana hapa hapa, Mambo ya kutoka nje huku maprodyuza wetu wanafanya kazi nzuri sioni kama ni kitu kizuri kwa sasa, binafsi kazi nyingi nitafanya Bongo”, alisema Vee Money.

Kwa sasa msanii huyo yupo nchini China akiwa na mpenzi wake Juma Jux, ambaye juzi alisaini mkataba na kampuni ya mitindo Vendome kutokana na lebo yake ya ‘African Boy’.

Comments

Comments are closed.

More in Burudani