Burudani

Tetezi juu ya Uchebe na Shilole kuachana

0
Tetezi juu ya Uchebe na Shilole kuachana
Uchebe na Shilole

Msanii wa muziki Bongo Fleva ambaye kwa sasa amejikita zaidi katika ujasiriamali, anaefahamika kwa jina la Shilole, baada ya kuwepo kwa tetezi nyingi juu ya kuvunjika kwa ndoa yake na Uchebe, hatimaye Uchebe amefunguka kuhusiana na hilo.

Uchebe amesema kuwa ni kweli akaunti ni yake ambayo ua jeusi lilipostiwa na kusindikizwa na maneno yaliyoleta utata na kutafsiriwa kuwa ndoa yao imevunjika kama ambavyo uhusiano wa Diamond na Zari ulivyovunjika.

Uchebe amefafanua kuwa watu wasiojulikana waliiba akaunti yake na kufanya hayo ambayo yamefanyika na kutafsiriwa hivyo na mashabiki. vile vile yeye na mke wake shilole wamewatoa hofu wananchi na mashabiki wao kua hawawezi kuachana na hawafikirii kuachana milele na pia ameongezea yupo sawa na mke wake hawajagombana kama ambavyo watu wanafikiria.

Soma pia:  Ommy Dimpoz amsamehe Steve Nyerere

“Sio kweli sijaachana na mke wangu na wala hatufikirii kuachana, kuna watu wanafiki wanapenda kusikia tumeachana, kuhusu ile post kuna mtu alifanikiwa kuhack acount yangu na kupost vile lakini sijamuacha mke wangu, na wala hatuna ugomvi, na niwaambie tu kuwa hatuachani leo hata kiama”, amesema Uchebe.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa mwishoni mwa mwaka jana, Ndoa yao ni moja kati ya ndoa ambazo zilifanya vizuri na kuvuma sana mitandaoni, huku ikiwa imehudhuriwa na wasanii mbalimbali.

Comments

Comments are closed.

More in Burudani