Burudani

Sera za Uhamiaji za Trump kumgusa 21 savage

0
Sera za Uhamiaji za Trump
Trump na 21 Savage

Sakata la kukamatwa kwa rapa maarufu nchini Marekani, 21 Savage kila kukicha linachukua sura mpya ambapo licha ya kuachiwa juzi mpaka itakaposomwa hukumu yake lakini kukamatwa kwake huko kumehusishwa na Rais wa Marekani, Donald Trump.

21 Savage alikamatwa wiki mbili zilizopita na maofisa wa uhamiaji wa Marekani, ikielezwa siyo raia wa nchi hiyo, nyumbani kwao ni Uingereza na anaishi Marekani kinyume na sheria.

Imeelezwa kuwa kilichojiri kwa Savage ni matokeo ya Trump kubadili taratibu za masuala ya uraia na uhamiaji na zoezi hilo limeanza kufanyiwa kazi kwa wasanii akitaka kusafisha eneo hilo na bahati mbaya imeanzia kwa Savage ambaye makabrasha yanaonesha si mzaliwa wa Marekani lakini aliingia nchini humo akiwa na umri wa miaka saba na sasa ana umri wa miaka 26.

Soma pia:  Ibrahimovic Aanza makeke Marekani

Taarifa nyingine inaeleza kuwa katika kesi hiyo maofisa wa uhamiaji hawatajumuisha kesi nyingine za jinai alizonazo mwanamuziki huyo ikiwemo ile ya dawa za kulevya na kama watafanya hivyo inaelezwa itaongeza uwezekano mkubwa wa Savage kutimuliwa Marekani.

Comments

Comments are closed.

More in Burudani