Michezo

Mohamed Salah awaangukia mashabiki

0
Mohamed Salah awaangukia mashabiki
Mohamed Salah

Straika wa Misri, Mohamed Salah amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kutokana na kutolewa mapema kwa timu yake ya Taifa kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Russia.

Misri iliaga michuano hiyo juzi baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Saudia Arabia kwenye mchezo uliofanyika Uwanja wa Volgogrand Arena, chini Russia.

Misri iliondoshwa kwenye michuano hiyo kwenye hatua za makundi bila ya poini hata moja pamoja na Mohamed Salah kufunga mabao mawili ambayo hayakusaidia kitu lakini ameweka rekodi kwenye fainali za mwaka huu.

Nyota huyo anayeichezea Liverpool, alisema anawaomba radhi mashabiki wa Misri kwani anaamini msimu ujao watafanya vizuri zaidi.

Alisema kuwa wachezaji wengi hawakuwa tayari kucheza kwenye michuano ya mwaka huu lakini anaamini wataenda kujipanga upya kwajili ya fainali za msimu ujao.

Soma pia:  Alsisi ashinda tena urais Misri

“Ninaomba radhi kwa mashabiki wa Misri baada ya timu yetu kutolewa mapema hatua ya makundi, wachezaji wengi hawakuwa tayari kucheza kombe la Dunia hivyo tunaenda kujipanga upya kwajili ya msimu ujao,” alisema Mohamed Salah.

Mohamed Salah Kombe la Dunia
Mohamed Salah

Comments

Comments are closed.

More in Michezo