Top Stories

Tundu Lissu Akihutubia kwa Mara ya Kwanza

0
Tundu Lissu Akihutubia
Mbunge Tundu Lissu

Mbunge Tundu Lissu akihutubia mbele waandishi wa habari nje ya hospitali Nairobi, Kenya Mbunge Tundu Lissu ameongelea mambo mbali mbali na waandhishi hao ikiwemo kuhusu watu waliomshambulia Septemba 7 mwaka jana.

Tundi lissu alisema kuwa, watu hao walioshambulia akiwa nyumbani kwake Area D, Dodoma walikuwa na uhusiano na serekali ya Tanzania na anaamini kuwa shambulio hilo dhidi yake lililenga kumnyamazisha kutokana na uokosoaji wake wa mara kwa mara wa serikali ya Tanzania.

Tundu Lissu ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati kwani hali nchini Tanzania imebadilika na kuwa taifa ambalo hakuna aliye salama.

Mawakili wanaweza kurushiwa mabomu kwa kuwawawkilisha wateja wao. Nchi ambayo afisi za mawakili zinaweza kuvamiwa, na mawakili kufungwa jela

Soma pia:  Tundu Lissu alivyowasili Brussels Ubelgiji

Mbunge huyo wa Singida Mashariki amesema kuwa kwa sasa Afya yake imeimarika sana, ikilinganishwa na hapo awali wakati anafikishwa hospitalini hapo kwa mara ya kwanza na kwamba anashukuru Mungu na wote waliomtakia uponaji wa haraka.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories