Michezo

Okwi kuwa Balozi wa Mbeya Tulia Marathon 2018

0
Okwi kuwa Balozi Tulia Marathon
Emmanuel Okwi

Emmanuel Okwi ameteuliwa kuwa Balozi wa Mbeya Tulia Marathon 2018, inayotarajia kufanyika Mei 6, Mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine, Jijini Mbeya.

Mbeya Tulia Marathon inayoasisiwa na Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson itawakutanisha wanariadha wa mbio za kilomita 42, kilomita 21, kilomita 150 kukimbia na baiskeli.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam jana, Mratibu na balozi wa Tulia Trust, Hassan Ngoma alisema Okwi ameteuliwa kuwa Balozi ili kunogesha mbio hizo.

Ngoma alitaja ada kwa washiriki kuwa ni Sh. 30,000 kwa washiriki wa mbio za km 42, Sh. 20,000 kwa km 21 na kukimbia na baiskeli na vingine ni Sh. 10,000 ambapo malipo yatatumwa kwa Tigopesa, Mpesa na Airtel Money.

Soma pia:  Emmanuel Okwi: Ninataka Ubingwa ligi kuu bara

Aliongeza kuwa mshindi wa kwanza wa km 42 atapatiwa sh. 3,000,000, na wa km 21 atapatiwa sh. 2,000,000 na mshindi wa kukimbia na baiskeli atapewa  sh. 2,000,000.

Mbali na Okwi mabalozi wengine wa Tulia Trust ni Mtangazaji wa Clouds, Babra Hassa, Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Lameck Ditto na Msanii wa Muziki Nancy.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo