Top Stories

Mashua ya plastiki ya Kenya kufanya safari ya kihistoria

0
Mashua ya plastiki
Mashua ya plastiki

Mashua iliyotengenezwa kwa kutumia mabaki ya plastiki yaliyokusanywa kutoka fukwe za Kenya, mwezi ujao inatarajiwa kufanya safari yake ya kwanza ikitokea kwenye mji wa Lamu kuelekea visiwani Zanzibar nchini Tanzania.

Boti hio itasafiri umbali wa kilometa zaidi ya 500 na itasimama katika visiwa kadhaa ili kueneza ujumbe kuhusu madhara yanayotokana na matumizi ya plastiki katika bahari.

Katibu mkuu wa mazingira nchini Kenya, Ali Noor Ismail amesema mazingira ya fukwe nyingi za bahari Afrika yamekuwa yakichafuliwa kwa plastiki, hatua ambayo imekuwa na madhara makubwa kwa viumbe hai baharini.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Ukanda wa Pwani, Juliette Biao amesema mpango huu wa kulinda mazingira ya bahari, unafaa kuigwa na mataifa mengine ulimwenguni.

Soma pia:  Uganda, Rwanda, Burundi kuanza kutumia passport za kielektroniki

Mmoja wa waliounda mashua hiyo, Hassan Shafi amesema kilichowavutia katika ubunifu huu ni takataka nyingi za plastiki ambazo zimekuwa zikipatikana katika mazingira ya bahari.

Mashua hiyo iliyoundwa na kikundi cha Plastic Revolution ilitengenezwa Kisiwani Lamu kwa kutumia plastiki na sasa iko safarini kuelekea visiwa vya Pemba na Unguja nchini Tanzania.

Katika siku chache zijazo, mashua hiyo itakamilisha safari ya Pemba na Unguja na kurejea ilipotoka ambapo mafundi watajaribu kutafakari zaidi kuhusu namna bora ya matumizi ya mashua hiyo.

Mashua ya plastiki Lamu Kenya
Mashua ya plastiki Lamu Kenya

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories