Michezo

Kamati ZFA Zanzibar yasubiri ripoti ya waamuzi

0
Kamati ZFA Zanzibar
Alawi Haidar Foum

Kamati ya kusimamia mashindano na ligi ya ZFA Taifa imesema inasubiri ripoti ya waamuzi itakayoelezea sababu ya kutofika uwanjani kuchezesha mechi kati ya Idumu na Kizimkazi.

Mechi hiyo ilipangwa kuchezwa Bungi, lakini haikufanyika baada ya waamuzi kutofika wakidaiwa kukosa nauli ya kuwafikisha hulo.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano timu mwenyeji ndio inayopaswa kutoa nauli na kuwapa waamuzi siku moja kabla ya mchezo lakini hilo halikufanyika kwa timu ya Idumu ambayo ndio ilikuwa mwenyeji.

Katibu wa kamati hiyo Alawi Haidar Foum (pichani) alisema kuwa wao mpaka sasa wanachojua mechi haikuchezwa kwa sababu waamuzi hawakufika hivyo baada ya ripoti ndo watajua kilichowafanya wasifike kwenye kituo.

Alisema kuwa hata hivyo kitendo walichokifanya cha kutofika uwanjani kwa madai ambayo wanayasikia si cha kiingwana na hakiwezi kuvumilika.

Soma pia:  Ligi ya ZFA Zanzibar kukosa Wadhanini

“Mimi nawashangaa hawa waamuzi kama wao wameshindwa kwenda kwa sababu ya nauli nadhani walikusudia kwa sababu wao kabla ya kuamua hilo wangewasiliana na sisi tuone cha kufanya,” alisema.

Aidha alisema, kama ni suala la nauli uongozi wa Idumu siku zote hutoa nauli wanapofika uwanjani hivyo waamuzi hawakutenda haki.

“Idumu hawajafika je hawana fedha za kukopeshana kama deni waamuzi wanaidai FA mbona wanachezesha ije kuwa 20,000 lazima watajibu na hawakututendea haki”, alisema Foum.

Nauli kutoka Mjini mpaka Bungi ni kati ya Sh 10,000 hadi 15,000, na waamuzi walioshindwa kufika ni Ramadhan Kombo, Iddi Khamis Mberwa, Nassir Msomali na kamisha wa mchezo huo ni Haji Majid.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo