Michezo

Bondia Lomachenko amvunja pua Crolla

0
Lomachenko amvunja pua Crolla
Vasyl Lomachenko

Bondia wa kimataifa wa Ukraine, Vasyl Lomachenko, juzi usiku aliibuka na ushindi dhidi yamkali wa masumbwi jijini Manchester, Anthony Crolla kunako raundi ya nne na kutwaa ubingwa wa dunia uzani ‘light,’ katika pambano lililopigwa jijini Manchester.

Utabaki kuwa ni usiku mchungu na wa kukumbukwa kwa Anthony Crolla, ambaye hakuishia tu kupoteza pambano hilo, bali kuvunjika pua na kushindwa kuendelea na mtifuanohuo uliochezeshwa na mwamuzi Jack Reiss.

Kwa ushindi huo, Lomachenko, anakuwa na rekodi ya kushinda mapambano 10 kwa KO, katika ushindi wake wa mapambano 13, kati ya 14 aliyopigana katika kipindi chake cha masumbwi ya kulipwa. Ni ushindi uliompa taji la WBA.

Vasiliy Lomachenko dhidi ya Anthony Crolla
Vasiliy Lomachenko dhidi ya Anthony Crolla
Soma pia:  Russia yawatimua wanadiplomasia wa Marekani

Comments

Comments are closed.

More in Michezo