Top Stories

Biashara yaongezeka kati ya Urusi na China

0
Urusi na China
Urusi na China

Biashara kati ya Urusi na China kwa Januari mwaka huu kimepanda kwa asilimia 10.8 kwa kiwango cha mwaka cha dola za Marekani bilioni 9.2.

Ripoti ya Kituo cha Forodha cha China imebainisha kuwa kiwango cha bidhaa zinazosafirishwa na China kwenda Urusi kimepanda kwa asilimia 11.5 katika mwezi huo wa Januari na kuzidi kwa dola za Marekani bilioni 4.3.

Kiwango cha bidhaa kinachopelekwa China kutokea Urusi kimepanda kwa asilimia 10.2 na kuwa dola za Marekani bilioni 4.89.

Mwaka jana kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili kilipanda kwa asilimia 27.1 na kufikia dola za Marekani bilioni 107.

Soma pia:  Rihanna na Jay Z waibuka tena pamoja

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories