Burudani

Rihanna na Jay Z waibuka tena pamoja

  0
  Rihanna na Jay Z wakiwa pamoja
  Rihanna na Jay Z wakiwa pamoja

  Baada ya kupita kipindi kirefu bila ya kuonekana pamoja, juzi Rihanna na Jay-Z wamekutana katika moja ya mikutano ya kibiashara Los Angeles na kuibua hisia nzito kwa mashabiki wao.

  Kwa mujibu wa watu wa karibu na nyota hao, wamedokeza kuwa baada ya kukutana, kati ya vitu muhimu walivyojadili ni kurejea kufanya tena nyimbo za pamoja kama walivyofanya hivyo miaka ya nyuma na kutingisha dunia.

  Mkongwe Jay-Z alimpa ushirikiano mkubwa Rihanna na wakati anatoka kimuziki akiwa kama bosi wa mwanadada huyo lakini pia kuingiza mashairi yake katika baadhi ya nyimbo kama Umbrella, Talk That Talk na Run This Town.

  Rihanna hajatoa wimbo mpya kwa takriban miaka miwili na inaelezwa kwa sasa yupo studio anaandaa vitu vipya na inawezekana kukutana na Jay-Z kukazaa kitu kipya.

  Soma pia:  Mapato kutokana na utalii kuongezeka Urusi
  Jay Z na Rihanna wakiwa pamoja
  Jay Z na Rihanna wakiwa pamoja Los Angels

  More in Burudani