Burudani

Ben Pol alalamika Mauzo ya Albamu

0
Ben Pol alalamika Mauzo ya Albamu
Ben Pol

Mkali wa miondoko ya R&B, Benard Paul ‘Ben Pol’ ametoboa siri kwamba hakuna faida yeyote aliyoipata katika utoaji wa Albamu yake.

Pia, amewaimba mashabiki kuwa wazalendo katika kutoa ushirikiano kwa wasanii wanao wapenda kununua kazi zao ili waweze kufika malengo.

Akizungumza na mwandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Ben Pol alisema kuwa sapoti ndio kitu muhimu kitakachowafanya wasanii wazidi kutoa albamu huku hakuna faida wanayoipata.

“Bado ni changamoto ukweli nasema, kwa sababu tukiongelea albamu yangu ya zamani 2011 mauzo yake yaliyonifikia mimi ni sawa sawa na ‘show moja’ ninayofanya”.

Hapa katikatiilikuwa shida ipo kwetu sisi wasanii hatutoi albamu lakini sasa hivi tunatoa na shida hizo zimehamia kwa watu, tunaomba watuunge mkono,” alisema Ben Pol.

Soma pia:  Albam mpya ya Neyo iko njiani

Hata hivyo Ben Pol alisema watu wanatakiwa wajifunze kuthamini vya kwao na kuvipenda. Alisema kama wanampenda Ben Pol basi wanapasw wanunue CD yake.

“Ukinunua CD ni njia moja wapo ya kumsapoti msanii unayempenda na kumpa Morari ya kutosha ili aweze kutengeneza albamu nyingi zaidi, tena yenye kiwango zaidi,” alisema.

Comments

Comments are closed.

More in Burudani