Top Stories

10 kortini kwa kufanyakazi bila vibali

0
10 kortini kwa kufanyakazi bila vibali
Kortini

Wafanyakazi 10 raia wa kigeni wenye asili ya Asia wa Kampuni ya Ortelo Business Corporation (OBC) inayofanya uwindaji katika eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro Mkoa wa Arusha, wamepandishwa kizimbani kwa kufanya kazi kinyume cha sheria za ajira kwa wageni.

Wakisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana, Niku Mwakatobe, Mwendesha Mashtaka wa Idara ya Kazi mkoani hapa, Immanuel Mweta alidai Novemba 2018 hadi Januari 2019, washtakiwa hao walitenda kosa la kufanya kazi kinyume cha sheria ya kuratibu ajira za wageni.

Mweta aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Darweshi Jumma, Riaz Aziz Khan, Mohammad Tayyab, Ali Bakhash, Abdulrahman Mohammed, Martin Crasta, Imtiaz Feyaz, Arshad Muhammad, Hamza Sharif na Zulfiqar Ali.

Soma pia:  Mbaroni kifo cha mwanaharakati

Alisema washitakiwa hawa wanashitakiwa kwa kosa la kufanya kazi kinyume cha sheria za uratibu wa wageni na kutokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.

Washtakiwa hao ambao walikuwa hawajui lugha ya Kiswahili wala Kiingereza na kutumia mkalimani aliyetambulika kwa jina la Muazamu Hussein, walikana makosa yao na kusema kampuni hiyo iliwaleta bila wao kujua chochote na wana uhakika na vibali walivyo navyo.

Washtakiwa hao walikuwa wakiwakilishwa na mawakili wawili, Godluck Peter akisaidiana na Daud Haraka, Wakili Haraka aliiomba mahakama kuwapatia dhamana washtakiwa hao kwani kosa linalowakabili linastahili dhamana.

Wakili wa upande wa mashtaka, Mweta alidai hawana pingamizi lolote juu ya dhamana ya washtakiwa ila dhamana ifuate utaratibu wa mahakama.

Hakimu Mwakatobe alisema dhamana kwa washtakiwa wote ipo wazi na kila moja anapaswa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho na vitambulisho na mali kauli ya thamani ya Sh milioni tano.

Soma pia:  Mbaroni kifo cha mwanaharakati

Washtakiwa hao walikidhi dhamana na wapo nje na kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 22, mwaka huu itakapotajwa tena.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories