Top Stories

Wabunge Venezuela wawekewa vikwazo

0
Wabunge Venezuela wawekewa vikwazo
Mjumbe wa Marekani anayehusika na masuala ya Venezuela, Elliott Abrams,

Marekani imewawekea vikwazo wabunge wa Venezuela kutosafiri kwenda nchini humo. Mjumbe wa Marekani anayehusika na masuala ya Venezuela, Elliott Abrams, alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari kuwa Washington imefuta viza kwa maofisa kadhaa wa Venezuela kama sehemu ya kumshinikiza Rais wa nchi hiyo, Nicolas Maduro kujiuzulu.

“Tunaweka vikwazo vya viza na kufuta viza za wabunge wasio halali,”alisema Abrams. Katika mkutano huo, Naibu Msemaji wa Ikulu, Robert Palladino, alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, atajadili suala la Venezuela na viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa ziara yake hivi karibuni Ulaya.

Wakati huo huo, mmoja wa Makamanda Wakuu wa Jeshi la Marekani, Craig Faller, alisema Jeshi la Marekani liko tayari kulinda wafanyakazi wa Marekani na vituo vya kidiplomasia nchini Venezuela litakapohitajika.

Soma pia:  Mkutano kutatua mgogoro Libya

Januari 23 mwaka huu, Rais wa Marekani, Donald Trump, alisema Marekani inamtambua kiongozi wa upinzani, Juan Guaido kama rais wa mpito wa Venezuela kauli iliyotolewa baada ya Maduro kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo.

Kujibu mapigo, Maduro alitangaza kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na kisiasa na Marekani na kuamuru maofisa wa kidiplomasia wa Marekani kuondoka humo ndani ya saa 72

Maandamano Venezuela
Hali ya kisiasa nchini Venezuela

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories