Top Stories

Urusi kupunguza uzalishaji mafuta

0
Urusi kupunguza uzalishaji mafuta
Uzalishaji wa Mafuta Urusi

Urusi imepanga kupunguza uzalishaji wa mafuta ghafi kati ya mapipa 90,000 hadi 100,000 kwa siku kuanzia mwezi huu. Waziri wa Nishati wa Urusi, Alexander Novak alisema kiwango hicho ni zaidi ya kilichopunguzwa Oktoba mwaka jana.

Nchi zinazoongoza kusafirisha mafuta duniani (OPEC) zilichukua hatua ya kupunguza uzalishaji mafuta Oktoba mwaka jana ikiwa ni kutekeleza makubaliano yao.

“Tulipanga Februari mwaka huu tupunguze uzalishaji wa mafuta kati ya mapipa 90,000 na 100,000 kwa siku. Tunajitahidi kufikia malengo yetu hayo. Ukilinganisha na Desemba, uzalishaji wa mafuta ushuke kwa mapipa 140,000 hadi 150,000 kwa siku,”alisema.

Novak alisema itakuwa mapema sana kusema kama mpango huo wa OPEC utaongezewa muda au la.

Nchi za OPEC zimekubaliana kupunguza uzalishaji wa mafuta kuanzia mwaka 2017 lakini makubaliano hayo yalisogezwa mbele mara mbili.

Soma pia:  Mwandishi auawa Mexico akipata kifungua kinywa

Desemba mwaka jana nchi hizo zilikubaliana kupunguza uzalishaji wa mapipa milioni 1.2 ya mafuta ghafi kwa siku, ili kuepuka kusambaza mafuta mengi kwenye soko kutokana na Marekani kuongeza uzalishaji na kuregezwa kwa vikwazo ilivyowekewa Iran.

Mpango wao nchi za OPEC zipunguze uzalishaji mafuta kwa mapipa 800,000 kwa siku na nchi zisizo mwanachama wa OPEC zipunguze kwa mapipa 400,000 kwa siku.

Urusi kiujumla itapunguza mapiga 230,000 kwa siku. Mpango huo ni wa nusu mwaka huu na itapitiwa upya Aprili. Waziri huyo alisema Januari Urusi ilipunguza uzalishaji wa mapipa 47,000 kwa siku ikilinganishwa na ilivyopunguza Oktoba mwaka jana.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories