Makala

Fahamu njia bora za kupanga Fridge ‘jokofu’ lako

0
Fahamu njia bora za kupanga Fridge
Jokofu

Unapotaka kufanya manunuzi, kitu cha kwanza unachotamani ni kutaka kupanga bidhaa zako zote zinazostahili kukaa kwenye jokofu, tena mara nyingine vitu wakati jokofu ni dogo.

Lakini amini ukipanga kila kitu katika jokofu katika sehemu husika utaokoa muda mwingi na fedha.

Zifuatazo ni baadhi ya kanuni zinazoweza kukusaidia kuweka jokofu lako katika hali nzuri.

Kuna baadhi ya sehemu katika jokofu ni baridi kuliko zingine shelfu za chini za jokofu huwa ni baridi zaidi, wakati shelfu za juu sio baridi sana kwa jokofu la mtindo huu na kuna jokofu zingine sehemu yenye baridi ama barafu huu sehemu ya juu na chini sehemu zisizokuwa na baridi .

Unashauriwa kuweka vinywaji na viporo katika shelfu ya juu wakati nyama mbichi sehemu ya chini lakini kwa aina nyingine za majokofu sehemu ya baridi huwa juu kabisa na mlango tofauti, hivyo unatakiwa kuweka huko nyama na bidhaa zingine mbichi zinazohitaji barafu.

Soma pia:  Fahamu namna ya kukabili moto wa jikoni

Kamwe usiweka maziwa au mayai katika mlango wa jokofu kwani ni sehemu katika jokofu isiyokuwa na baridi kabisa, weka kwenye shelfu la chini mwishoni kabisa.

Mara nyingi huwa tunatupa vyakula kutokana na utaratibu mdogo, hivyo unashauriwa ukileta bidhaa za vyakula na matumizi ya nyumbani, vipya visogeze nyuma halafu vilivyokuwepo visogeze mbelea.

Hii itakusaidia kula bidhaa za zamani kabla hazijaharibika na ukajikuta unazitupa.

Njia nyingine ya kuokoa nafasi katika jokofu ni kufahamu nini hasa unataka kuweka katika jokofu.

Usiweke nyanya, viazi au mkate kwenye jokofu. Pia vitunguu au mafuta. Kuweka vitu hivi katika jokofu vitaondoa ladha na kuviharibu, lakini pia vitatoa nafasi kwa bidhaa zingine zinazopaswa kuhifadhiwa katika jokofu

Kupangilia vyakula Jokofu
Upangiliaji wa vyakula katika Jokofu

Comments

Comments are closed.

More in Makala