Top Stories

Riek Machar kurejea Sudan Kusini Mei

0
Riek Machar kurejea Sudan Kusini Mei
Dk Riek Machar

Makamu wa kwanza wa Rais wa Sudan Kusini, Dk Riek Machar amesema atarejea nchini mwake Mei mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya mkataba wa amani waliosaini na rais wa nchi hiyo Salva Kiir, mwaka jana.

Katika mkataba huo, kiongozi huyo wa waasi anarejea katika nafasi yake ya awali kama makamu wa kwanza wa rais akishirikiana na mawaziri wanane.

Katika makubaliano hayo, serikali ya mpito inatakiwa kuanza kazi Mei mwaka huu, ikiwa ni mwisho wa miezi minane ya kamati ya maandalizi ya serikali hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Mkuu wa Ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), David Shearer, alisema Machar amewahakikishia kurejea nchini humo Mei mwaka huu.

Soma pia:  Biashara yaongezeka kati ya Urusi na China

Alisema ingawa bado kuna masuala ambayo hayajafanyiwa kazi makubaliano hayo ya amani yametoa nafasi kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuua maelfu na wengine kukimbia nchi yao.

Oktoba mwaka jana, Machar alirejea Juba kushiriki hafla ya kiserikali kuhusu mkataba wa amani, hafla iliyohudhuriwa na viongozi wengi wa ukanda huo.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories