Top Stories

Nigeria yasogeza mbele uchaguzi

0
Nigeria yasogeza mbele uchaguzi
Uchaguzi Nigeria

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Nigeria (Inec) imesogeza mbele tarehe ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge nchini humo hadi Februari 23 mwaka huu. Awali uchaguzi huo ulikuwa ufanyike jana.

Inec ilitangaza uamuzi huo juzi na kusema wamechukua uamuzi huo ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki unafanyika.

“Tumesogeza mbele tarehe ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge hadi Februari 23 mwaka huu, tunataka uwe huru na wa haki, hivyo maandalizi ya tarehe ya awali yameahirishwa”,alisema Mwenyekiti wa Inec,Mahmood Yakubu.

Wakati uchaguzi wa rais na wabunge ukipangwa kufanywa Februari 23, mwaka huu ule wa magavana, makansela na bunge kuu umepangwa kufanywa Machi 9, mwaka huu.

Mabadiliko hayo ya uchaguzi yamejiri baada ya kuwepo na kikao cha dharura cha tume hiyo mjini hapa.

Soma pia:  Marekani yatakiwa kuondoka Syria

Vyama viwili vikubwa vya siasa nchini hapa cha APC na PDP vimeshutumiana kila mmoja akimtuhumu mwenzake kujipanga kufanya njama za kuiba kura.

Rais Muhammadu Buhari wa chama tawala cha APC, amewataka Wanaigeria wote kuwa watulivu na kuonesha uzalendo kwa kuungana na kufanya uchaguzi wa haki na huru.

Vituo vya uchaguzi nchini humo viko zaidi ya 120,000 na wagombea 73 wanawania urais dhidi ya Rais Buhari ambaye kama atashinda itakuwa muhula wake wa pili.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories