Top Stories

Mzee Majuto atoka Hospitali ya Muhimbili

0
Mzee Majuto atoka Hospitali ya Muhimbili
Mzee Majuto alipokuwa Hospitali

Mchekeshaji, Amri Athumani maarufu kama ‘Mzee Majuto’ ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kurejea akitokea nchini India.

Mzee Majuto, alilazwa hospitalini hapo tangu Januari mwaka huu baada ya hali yake kubadilika ghafla na Mei 5, mwaka huu alipewa rufaa kwenda nchini India katika Hospitali ya Apollo kwajili ya matibabu zaidi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano kwa Umma, MNH, Neema Mwangomo alithibitisha kuruhusiwa kwa Mzee Majuto.

“Mzee Majuto aliruhusiwa juzi jioni kurudi nyumbani baada ya afya yake kuimaika,”Alisema.

Ofisa wa Habari wa Chama cha Waigizaji wa Wilaya ya Kinondoni, Masoud Kaftani, alisema Mzee Majuto alisharuhusiwa hospitali hvyo yupo nyumbani kwa sasa.

Alisema wamemweka Mzee Majuto katika sehemu maalumu ambayo hawana mpango wa kuitaja kwa sasa ili kuhakikisha anapumzika na hali yake inaimarika zaidi.

Soma pia:  Ommy Dimpoz amsamehe Steve Nyerere

“Mzee Majuto yupo nyumbani na tumemweka sehemu ambayo hataonana na watu wengi kwa muda ili kuhakikisha anapata muda wa kupumzika na afya yake kuimarika zaidi,” alisema Masoud Kaftani.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories