Top Stories

Mwandishi wa Daily Nation Kenya apokea vitisho

0
Mwandishi wa Daily Nation Kenya apokea vitisho
Justus Wanga

Mwandishi wa gazeti la Daily Nation nchini Kenya, Justus Wanga (Pichani) ameeleza kuwa amepokea vitisho siku ya jumapili kutoka kwa David Mugonyi ambaye ni msemaji wa Makamu wa Rais, William Ruto, hio ni baada ya kuandika makala kuwa kuna ugomvi mkubwa kati ya Rais na Makamu wake, kutokana na uteuzi wa Baraza la Mawaziri.

I want to be outright with you (Ninataka kuwa wazi na wewe), Ukitaka kufutwa kazi, continue with that path (endelea na njia hio) , utafutwa, utafutwa, sikudanganyi, utafutwa,” David Mugonyi alisikika akimwambia maneno hayo Justus Wanga kwa njia ya simu ya sekunde 50.

Na pia katika Mfulululizo wa ujumbe wa maandishi, David Mugonyi alimshtaki Justus Wanga juu ya uandishi wa habari usiofaa, akidai kuwa ameandika habari za uongo juu ya makala hio.

Soma pia:  Nini kilitokea kwa Viongozi waliojiapisha wenyewe?

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories