Top Stories

Mwandishi auawa Mexico akipata kifungua kinywa

0
Mwandishi auawa Mexico
Mwandishi wa Habari, Jesus Ramos Rodriguez

Maofisa wa Mexico wamethibitisha kuwa Mwandishi wa Habari, Jesus Ramos Rodriguez (Pichani) ameuawa na watu wasiojulikana wakati akipata kifungua kinywa katika hoteli moja mjini Tabasco juzi.

Tukio la mauaji hayo ya mwandishi wa habari nchini humo linafanya matukio hayo kuwa mawili tangu kuanza kwa mwaka huu.

Mwandishi huyo alikuwa mtangazaji wa Radio anayeendesha vipindi viwili vinavyorushwa na radio nchini humo kila siku.

Serikali nchini humo imetoa taarifa ikisema inalaani mauaji hayo na kusema itaongeza ulinzi kwa waandishi wa habari na kutaka haki za binadamu na kazi zao kulindwa.

Serikali ya mji wa Tabasco unachunguza tukio hilo na kusema hadi sasa mtuhumiwa wala sababu za mauaji hazijajulikana.

Mratibu wa Mawasiliano katika Ofisi ya Rais nchini humo, Jesus Ramirez aliweka kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ujumbe wa kutaka ulinzi dhidi ya wanahabari.

Soma pia:  Biashara yaongezeka kati ya Urusi na China

Katika mtandao wake huo alisema; ‘Uhuru wa kujieleza ni haki ya msingi na alama mojawapo wa uwepo wa demokrasia, haki na ukombozi.’

Mwaka jana nchini humo wanahabari wanane waliuawa na nchi hiyo inashika nafasi ya nne duniani kwa kuwa nchi hatari, kwa mujibu wa Mtandao wa Waandishi Wasio na Mipaka Kimataifa (RSF).

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories