Top Stories

Mgomo Makerere bado moto

0
Mgomo Makerere bado moto
Makamu Mkuu wa Chuo cha Makerere, Profesa Barnabas Nawangwe

Baada ya mgomo wa muda mrefu wa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Makerere kutoingia darasani, uongozi wa chuo hicho umevunja ukimya kwa kuwataka wahadhiri hao kuchagua moja kati ya mambo mawili.

Chuo hicho kimesema ama warudi darasani kufundisha na kumaliza mgomo huo rasmi au wachukuliwe hatua stahili ambapo watafukuzwa kazi.

Katika barua iliyoandikwa na uongozi wa chuo hicho kwenda kwa wafanyakazi wote chuoni hapo, uongozi umewataka wahadhiri ambao hawahudhurii darasani kufundisha, kuacha kufanya hivo.

“Viongozi wa vyuo, wakurugenzi, walezi wa wanafunzi na wakuu wa idara wanatakiwa kuchukua orodha ya wahadhiri watakaoingia darasani na kufundisha, kwa lengo la kuwatambua wale wote wasiotaka kuhudhuria ili wachukuliwe hatua stahiki,” ilisema barua hiyo iliyosainiwa na Meneja Rasilimaliwatu, Chuo Kikuu cha Makerere, Andrew Abunyang.

Soma pia:  Nini kilitokea kwa Viongozi waliojiapisha wenyewe?

Alisema wafanyakazi wote wanastahili kufika ofisini mapema saa 2:00 asubuhi siku ya Jumatano ambapo yatachukuliwa mahudhurio. Kwa mujibu wa Abunyang, yeyote atakayekiuka utaratibu huo atachukuliwa kuwa amejifukuzisha kazi mwenyewe.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Makerere, Profesa Barnabas Nawangwe alithibitisha kuwa barua hiyo imetoka chuoni hapo na akaongeza kuwa mtumishi wa chuo ambaye hatafuata masharti hayo atakuwa amejiondoa katika utumishi mwenyewe.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories