Top Stories

Mbunge mbaroni kwa Ubakaji

0
Mbunge mbaroni kwa Ubakaji
Kuldeep Singh Sengar

Polisi nchini India imemkamata Mbunge kutoka Chama tawala cha Bharatiya Janata (BJP), kwa mashtaka ya kumteka na kumbaka msichana mmoja mwaka uliopita.

Kuldeep Singh Sengar, mwanachama wa BJP kwenye Bunge la Jimbo la Uttar Pradesh, anatuhumiwa kwa kumbaka msichana wa miaka 16, Juni, mwaka Jana.

Kesi hiyo ilitawala vyombo vya habari vya kitaifa baada ya mwathirika kujaribu kujiua April 8, mwaka huu mbele ya makazi ya waziri mkuu wa jimbo hilo.

Siku moja baadaye baba yake alifariki dunia akiwa mikononi mwa polisi baada ya kupigwa na kaka wa Mbunge huyo, ambaye amekamatwa tagu wakati huo.

Hata hivyo Mbunge huyo ameyakana madai hayo akisema yamechochewa kisiasa. India imekuwa ikitawala vyombo vya habari miaka ya karibuni kutokana na matukio ya unyanyasaji kingono dhidi ya wanawake.

Soma pia:  Watu 17 wafa moto hotelini India

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories