Top Stories

Mapato kutokana na utalii kuongezeka Urusi

0
utalii kuongezeka Urusi
Mji Mkuu wa Urusi, Moscow

Kitendo cha Urusi kurahisisha upatikanaji wa viza kumetajwa kuwa kutaongeza mapato ya serikali ya nchi hiyo kutokana na utalii kwa kati ya asilimia 20 hadi 30.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Maendeleo ya Uchumi, Maxim Oreshkin.

“Kwa mujibu wa makadirio yetu, kurahisisha upatikanaji wa viza na kufanya mabadiliko mengine kutasaidia haraka kuongeza mapato yatokanayo na utalii ambayo kwa sasa tunapata dola za Marekani bilioni 10, hivyo yataongezeka kwa asilimia kati ya 20 na 30,” alisema na kuongeza: “Tutaendelea kusukuma mradi wa viza kielektroniki na maamuzi ya kuzidi kupunguza urasimu kwenye upatikanaji wa viza pamoja na nchi nyingine ili kuhakikisha nchi yetu inafaidika”.

Alisema Rais wa Urusi, Vladimir Putin anaunga mkono mabadiliko kwenye taratibu za upatikanaji wa viza.

Soma pia:  Waangalizi wa Urusi wazuiwa Ukraine

Oreshkin alisema kuwa Januari 30 mwaka huu, Rais Putin na mawaziri wake walijadiliana kuhusiana na mpango mkakati wa maendeleo ya utalii wa hadi mwaka 2015.

Mpango huo utawasilishwa ndani ya kipindi cha miezi miwili. Alisema kuna mpango wa kurahisisha upatikanaji viza, ruzuku ya kodi na kufadhili sekta ya utalii.

Kwa mujibu wa waziri huyo, kuna haja ya kuvutia zaidi watalii kuja Urusi na kuwashawishi warusi kutembelea vituo vya nchini humo badala ya kwenda nje ya nchi.

Vivutio vya Utalii Urusi
Mlima elbrus
Vivutio vya Utalii Urusi
Kisiwa cha Kizhi
Vivutio vya Utalii Urusi
Suzdal – Urusi
Vivutio vya Utalii Urusi
St Sophia Cathedral, Novgorod Urusi
Vivutio vya Utalii Urusi
Moscow Urusi
Vivutio vya Utalii Urusi
Makumbusho ya Hermitage
Vivutio vya Utalii Urusi
Moscow Kremlin – Urusi

 

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories