Top Stories

Mahausigeli kutoka Uganda washikiliwa Oman

0
Hausigeli kutoka Uganda washikiliwa Oman
Resty Namusisi (24) na Joyce Nanyonjo (20)

Wasichana wawili walioondoka nchini Uganda kwenda Oman kufanya kazi za ndani kupitia nchini Kenya wanashikiliwa katika taifa hilo la Kiarabu.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vya habari nchini Uganda zinasema kuwa msafirishaji haramu wa wasichana hao ni mwananchi wa Uganda.

Msafirishaji huyo haramu Issa Kisekka kutoka Manispaa ya Nansana katika Wilaya ya Wakisona alilipwa dola za Marekani 4,000 sawa na shilingi za Uganda milioni 14 na kampuni moja ya Oman ambayo ndiyo mpokeaji wa wasichana hao.

Mbali na kiasi hicho cha fedha kutoka katika kampuni hiyo ya Oman, Kisseka anadaiwa kupokea shilingi za Uganda milioni moja kutoka kwa kila msichana kama sharti la kuwapeleka Uarabuni.

Baada ya kupokea fedha hizo, Kisseka aliondoka na kuwaacha wasichana hao mikononi mwa kampuni hiyo ndipo uongozi wa familia inayomiliki kampuni hiyo ukawaambia wachague jambo moja kati ya mawili.

Soma pia:  Museveni awalaumu wanasiasa Uganda

La kwanza ni kufanya kazi hadi fedha zilizotolewa kwa Kisseka kumalizika yaani zile milioni 14 au kuwasiliana na wazazi wao kila mmoja alipe dola za Marekani 2,000 sawa na shilingi milioni saba.

Wasichana hao, Resty Namusisi (24) na Joyce Nanyonjo (20), wanadaiwa kushikiliwa katika sehemu salama katika mji mkuu wa Oman, Muscat.

Moja ya masharti wanayokabiliana nayo ni kufanya kazi hadi mkataba wao uishe

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories