Top Stories

Kampuni kulipwa mafuta kujenga barabara

0
Kampuni kulipwa mafuta kujenga barabara
Ujenzi wa Barabara Sudan Kusini

Serikali itaipatia kampuni ya ujenzi wa barabara kutoka China mapipa 10,000 ya mafuta yasiyosafi shwa kwa siku ili kujenga barabara nchini humo.

Uchumi wa nchi hiyo unategemea kwa kiasi kikubwa kusafirisha nje ya nchi mafuta ambapo baadhi ya visima vya mafuta vilisitisha shughuli zake kutokana na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe, lakini vilifunguliwa tena mwezi uliopita.

Naibu Waziri wa Habari, Lily Albino Akol alisema maamuzi hayo yamefanyika katika mkutano wa baraza la mawaziri uliofanyika wiki iliyopita.

Waziri huyo hakueleza mwisho wa kampuni hiyo ya China kusitisha kupewa mapipa 10,000, ambapo nchi hiyo kwa sasa inauza pipa moja dola za Marekani 61 katika soko la kimataifa.

Rais wa nchi hiyo, Salva Kiir katika ziara yake nchini China Agosti mwaka jana alikubali kutoa mafuta ghafi kwa kampuni kutoka china ili kujenga barabara.

Soma pia:  UN yasaidia Sudan Kusini kujikinga na ebola

Serikali imepanga kujenga barabara kutoka Nadapal mpaka Torit na Juba pia kutoka Juba mpaka Rumbek na Wau.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories