Makala

Jinsi Unavyoweza kukabiliana na Midomo mikavu

0
Midomo mikavu
Midomo mikavu

Baadhi ya watu wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la ukavu wa mdomo (lips) kitendo ambacho kinawakosesha raha na kuwafanya washindwe kujiamini.

Tatizo hili limekuwa likitokea kwa jinsia zote kwa wanawake na wanaume na mara nyingi umfanye mtu ajihisi kupoteza mvuto.

Watu wa jinsia zote hususani wafuatiliaji wa urembo na utanashati, huangaika mara kwa mara kutafuta njia au dawa inayoweza kuwasaidia kuondokana na tatizo hili bila kujua nini chanzo.

Kwa mujibu wa mtandao wa www.healthline.com umetaja sababu mbalimbali za midomo kukauka na hata kupasuka.

Sababu zilizotajwa ni upepo mkali, ukosefu wa virutubisho mwilini, magonjwa ya ngozi, upungufu wa maji mwilini na baadhi ya vipodozi vyenye kemikali.

Namna ya kutibu tatizo hilo la ukavu wa midomo (lips) kwa njia ya asili ni:

Soma pia:  Jinsi ya Kupamba chumba cha kulala

Unywaji wa maji

Kwa kawaida watalaamu wanashauri binadamu anywe maji kulingana na uzito wa mwili wake, lakini ili kufanya midomo yako ‘lipsi’ kulainika hakikisha unakunywa angalau glasi nane za maji kila siku ili kuboresha ngozi yako.

Matunda na mboga za majani

Matunda pia hususani yenye maji maji kama karoti, matango, nyanya na matikiti yanaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kukinga au kukabiliana na tatizo hili na kuimarisha afya ya ngozi yako kwa ujumla.

Mafuta ya mgando (Vaseline)

Paka mafuta ya mgando au samli katika midomo yako kila unapotaka kulala, hii itasaidia kufanya midomo yako iwe na unyevunyevu.

Lipbam

Hakikisha unatumia mafuta maalum za kupaka katika midomo yako hasa wakati wa baridi ‘lipbam’. Majani ya hiliki Tumia majani ya hiliki kusugua katika midomo yako hii itakusaidia kuzifanya ziwe laini zaidi.

Soma pia:  Fahamu njia bora za kupanga Fridge 'jokofu' lako

Mswaki

Sugua ngozi ya midomo yako kwa kutumia mswaki na maji ya uvuvugu angalau mara moja kwa wiki, hii itasaidia kuondoa seli zilizokufa katika ngozi ya midomo yako.

Limao na glycelin

Paka mchanganyiko wa maji ya limao na ‘glycelin’ katika ngozi ya midomo yako kila usiku, acha kwa usiku mzima hadi asubuhi ndipo uoshe, hii itakusaidia kung’arisha midomo yako.

Tui bubu la nazi

Lainisha ngozi ya midomo yako kwa kupaka tui bubu la nazi katika midomo yako.

Tiba ya Midomo mikavu
Midomo mikavu kabla na baada

Comments

Comments are closed.

More in Makala