Makala

Je Wajua? Wamakonde ndio walioanzisha Msasani

0
Wamakonde ndio walioanzisha Msasani
Fukwe za Msasani

Eneo la Msasani ni kata mojawapo katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam. Kata hii kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002, ina wakazi 43,457.

Ni eneo ambalo ndani yake kuna bahari na nyumba za kifahari ambapo watu wenye fedha wanaishi. Ni moja ya maeneo yenye hadhi ya juu ukiacha Masaki na Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kama ilivyo kwa maeneo mengine mengi nchini, majina yake yana chanzo chake, Msasani nayo ni vivyo hivyo.

Taarifa zinaeleza kuwa katika eneo hilo la Msasani kulikuwa na mzee maarufu aliyekuwa akiishi maeneo hayo aliyeitwa Mussa Hassan. Mzee huyo alipata wageni wengi kutoka mikoa ya Kusini, hasa Mtwara na wengine walitokea nchini Msumbiji.

Soma pia:  Top 5 ya Wachezaji ghali zaidi duniani 2017/2018

Simulizi zinabainisha kuwa, watu wa maeneo hayo hasa Wamakonde walipata shida sana kulitamka jina hilo la Mussa Hassan, lakini iliwabidi walitamke au hata wanapoelekezana na kutaka kupita eneo la mzee huyo, walikuwa wakisema Mchachani.

Lakini baadaye wakawa wanajitahidi kuliboresha ndipo likazaliwa jina la Msasani ambalo linatumika hadi leo.

Comments

Comments are closed.

More in Makala