Makala

Faida za Mdalasini, Mdalasini katika Urembo

0
Faida za Mdalasini
Mdalasini

Kila mwanamke anapenda kuonekana mrembo na nadhifu machoni mwa watu wengine, ndio maana baadhi hutumia gharama kubwa kujipendezesha, hata hivyo zipo njia za asili unaweza kutumia na ukang’arisha ngozi yako na kuonekana mrembo na kuvutia.

Mdalasini ni kiungo cha jikoni ambacho kimezoeleka kutumika katika mapishi ya chai, pilau na vyakula vingine mbalimbali vinavyotumia viungo.

Lakini mdalasini unaweza kuutumia kwa kung’arishia ngozi yako na kuondoa mabaka na chunusi usoni.

Namna ya kutumia Chukua mafuta ya mdalasini kusafishia uso kwa kutumia maji ya mvuke yaliyotiwa mafuta hayo.

Njia;

1) Chukua matone mawili au matatu ya mafuta weka kwenye bakuli la maji ya moto,

2) funika kichwa kwa kutumia taulo,

3) kaa kwenye mvuke mpaka uhakikishe unatoka jasho.

Soma pia:  Kamari inavyoliza maelfu na kumchekesha mmoja

Mvuke wa mafuta unasaidia kutibu chunusi na kumaliza kabisa tatizo hilo. Unaweza kufanya hivi mara mbili kwa wiki.

KUOGA MAJI YA MDALASINI.

Mafuta haya yanafaida mara mbili, kwanza yanakuwa na harufu nzuri lakini pia yanasaidia kuchangasha mwili pamoja na uwezo wa kulinda ngozi na bakteria.

Chukua matone sita vya mafuta changanya na chumvi ya kupikia nusu kikombe weka kwenye ndoo uliyoandaa kwa ajili ya kuogea .

JIKANDE KWA MAFUTA YA MDALASINI

Weka matone 10 ya mafuta katika milimita 250 ya maji ya moto, loweka taulo au kitambaa ndani ya maji hayo kisha jikande katika mwili wako hasa pale panapouma. Maji haya ni mazuri kwa kutibu michubuko ya ngozi, maumivu ya viungo au misuli na matatizo ya ngozi.

Comments

Comments are closed.

More in Makala