Top Stories

Dk. Shein mgeni rasmi mashindano vyuo vikuu

0
mgeni rasmi mashindano vyuo vikuu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mashindano ya Taasisi ya Elimu ya juu na Vyuo Vikuu Zanzibar (ZAHLIFE) yatakayoanza Juni 29, mwaka huu.

Akizungumza mjini hapa katibu Mkuu wa Kamati ya Habari na michezo ya ZAHLIFE, Masud Juma Abdulrahman, alisema maandalizi kwa upande wa mashindano yameshakamilika na vyuo vyote tayari vimeshawasilisha majina ya wanafunzi watakaoshiriki michuano hiyo.

Masudi alisema mashindano ya Kombe la ZAHLIFE yapo kwa ajili ya kujenga uhusiano baina ya vyuo na taasisi hiyo ili kuondoa changamoto zinazoikumba elimu ya juu Zanzibar.

“Tumejipanga kuondoa lawama za mamluki kwenye mashindano haya,” alisema Masudi na kuianisha jumla ya vyuo 13 vinatarajia kushiriki katika mashindano hayo.

Soma pia:  Ligi ya ZFA Zanzibar kukosa Wadhanini

Alisema vyuo vitatu ambavyo ni Melisha Training, Zibret na Kizimbani vimejitoa katika mashindano hayo sababu ya kutingwa na mitihani.

Chuo kikuu cha Zanzibar (ZU) Kiliibuka bingwa wa mashindano hayo baada ya kukinyoa chuo cha Afya, huku upande wa wanawake Mwenge wakiibuka mabingwa wa mchezo wa nage kwa kukipa dozi Chuo cha Habari Zanzibar.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories