Makala

Jinsi ya kupata Passport mpya ya Kielektroniki

  0

  Last updated: July 14th, 2019.

  Je! unafahamu Jinsi ya kupata Passport mpya ya Kielektroniki Tanzania?

  Kitambulisho cha Taifa, kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ni moja ya viambatanisho muhimu ambavyo vitazingatiwa katika utaratibu mzima wa utoaji wa passport mpya za kielektroniki, Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Dr Anna Makakala Alisema.

  Mradi wa Pasipoti ya Kielektroniki pamoja Faida zake

  Passport ya Kielektroniki Tanzania

  Akizungumzia jinsi ya kupata pasipoti mpya ya kielekroniki kabla ya uzinduzi huo  katika makao makuu ya idara ya Uhamiaji Dar es Salaam, jana (jumatano). Dkt. Makakala alisema kuwa wale wote wanaotaka kupata pasipoti mpya ya kielektroniki wanatakiwa kuwa na Kadi ya Kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA.

  “Ikiwa unataka kuondokana na usumbufu usio na ulazima, utahitajika kuja na Kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA pamoja kujaza fomu husika katika ofisi zetu…. Na huduma hio ya kwa sasa inatolewa pekee katika ofisi zetu za Uhamiaji Dar es Salaam na Zanzibar pekee,” Alisema Dkt Makakala

  Soma pia:  Top 10 ya Nchi tajiri Afrika kwa GDP

  Aidha Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt Mwigulu Nchemba, alimpongeza Raisi katika kurasa yake ya tweeter kwa kuandika “Tunasonga mbele,Asante Mh. Rais J.P.Magufuli kwa hatua kubwa hii ya kuzindua hati ya kusafiri ya kielektroniki. Mkataba wetu na watanzania ni kuwaletea maendeleo chanya kadri Mungu atakavyotujalia,”

  Soma makala kwa lugha ya kiengereza inayoelezea masharti ya kuomba pasipoti pamoja na hatua utakazopitia katika maombi ya pasipoti mpya ya kielektroniki, bofya hapa.

  Tumia link za hapo chini kujua documents zinazohitajika wakati wa kuwasilisha maombi ya kupata passport mpya pamoja na gharama zake;

  Jinsi ya kupata Passport mpya ya Kielektroniki

  Passport mpya za Kielekroniki Tanzania

  More in Makala