Michezo

Ufaransa, Denmark zafuzu 16 bora Kombe la Dunia

0
Ufaransa Denmark zafuzu 16 bora
Kombe la Dunia 2018 nchini Russia

Timu ya taifa ya Ufaransa na Denmark zimefuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Russia.

Timu hizo zilipangwa kundi C, zimetinga hatua hiyo baada ya kufanya vyema huku Peru na Australia zikiaga michuano hiyo. Ufaransa imemaliza hatua ya makundi ikiwa kileleni kwa pointi saba baada ya kucheza mechi tatu huku Denmark ikimaliza nafasi ya pili na pointi tano.

Kwenye kundi hilo, Peru imeshika nafasi ya tatu ina pointi tatu huku Australia ikiburuza mkia na pinti moja. Kwenye kundi hilo, Peru imeshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu huku Australia ikiburaza mkia na pointi moja.

Katika mechi za mwisho zilizochezwa jana, Ufaransa ilitoka suluhu dhidi ya Denmark huku Peru ikiifunga Australia mabao 2-0. Mabao ya Peru yalifungwa na Adre Carrilo dakika ya 18 na Jose Paulo Guerrero katika dakika ya 50.

Soma pia:  Maradona amsaka aliyemzushia kifo

Timu hizo zimeungana na Uruguay, Ureno, Hispania na wenyeji Russia katika hatua inayofuata ya michuano ya Kombe la dunia msimu wa 2018 nchini Russia.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo