Michezo

Tetezi juu ya Uhamisho wa Riyad Mahrez

0
Tetezi juu ya Uhamisho wa Riyad Mahrez
Riyad Mahrez

Riyad Mahrez ni mchezaji anaewindwa na clubu kubwa nchini Uengereza mwezi huu baada ya kuonyesha uchezaji wa kiwango cha hali ya juu kwa clabu yake ya Leicester City kama ilivyoripotiwa na gazeti la The Sun.

Winga huyo kutokea clabu ya leicester City amefunga magoli saba (7) na pia kusababisha magoli saba (7) katika ligi kuu ya Uingereza, hiyo imesababisha Clubu ya Chelsea na Liverpool kutaka kumsaini ili ziweze kuimarika zaidi msimu huu.

Meneja wa Leicester City Claude Puel ameongea kwa kutilia mkazo kuwa Mahrez ataendelea kubaki katika Uwanja wa King Power mpaka mwisho wa msimu wa 2017/2018, lakini inaonyesha kuwa huenda Leicester wakazingatia dau la zaidi ya pauni millioni thalathini (£30 milioni) mwezi huu wa january.

Soma pia:  Pep Guardiola amuomba radhi Riyad Mahrez

Kwa mchezaji wa umri wa miaka 26 haitakuwa tatizo kwa Liverpool kuweza kumsaini ikiwa watafanikiwa kumuuza Philippe Coutinho kwenda Barcelona kwa dau la pauni millioni mia moja na arubaini (£140 milioni) kama wengi wanavyotajia.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo