Michezo

Paul Pogba amkubali sana Kocha Solksjaer

0
Pogba amkubali sana Kocha Solksjaer
Pogba na Solskjaer

Paul Pogba anahisi hali ya sasa ya Manchester United chini ya Ole Gunnar Solksjaer inafanana na ile ya chipukizi wa timu hiyo wa mwaka 1992.

Tangu Solksjaer alipombadili Jose Mourinho Desemba mwaka jana, United imepoteza mechi moja tu dhidi ya Paris Saint-Germain ambapo walifungwa mabao 2-0 kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Pogba anadhani uzoefu wa Solksjaer, unaweza kuisaidia Manchester United kuwa moja tena.

“Najaribu kutoa uzoefu wangu kwa wachezaji chipukizi kwa sababu nilipata nafasi ya kucheza kombe la Dunia, nimecheza kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na fainali ya Mataifa ya Ulaya,” alisema Pogba

“Hivyo najaribu kutoa huo uzoefu kwa vijana. Ni utamaduni wa klabu hii, toka kizazi cha David Beckham, Paul Scholes, Nicky Butt, Gary Neville.

Soma pia:  Sanchez atamani Ligi ya Mabingwa

“Unapotoka kwenye akademi unataka kucheza kwenye kikosi cha kwanza na kufanya mambo makubwa.

“Sasa una Marcus Rashford, bado kijana mdogo lakini mwenye kipaji sana na mchezaji wa kiwango cha juu na mimi na Jesse Lingard ambao tumecheza pamoja sijui kwa miaka mingapi.

“Niliwahi kusikia kwenye hii klabu hakuna umri. Ukiwa tayari kucheza, basi acha vijana wacheze na wathibitishe uwezo wao. Hivyo ndivyo ilivyo. Hii ni Manchester United. Una nafasi kwenye hii klabu.

“Wachezaji chipukizi wanakuja na kuthibitisha uwezo wao na kisha wanakuwa wachezaji wa kiwango cha juu kwenye kikosi cha kwanza.”

Comments

Comments are closed.

More in Michezo