Michezo

Maradona amsaka aliyemzushia kifo

0
Maradona amsaka aliyemzushia kifo
Maradano akiwa Uwanjani wakari Argentina ikichana na Nigeria katika hatua ya makundi.

Mshambuliaji wa zamani wa Argentina, Diego Maradona, ametoa ofa ya pauni 8,000 kwa yeyote atakayemnasa mtu aliyemzushia kifo.

Maradona mwenye umri wa miaka 57, alilazimika kutibiwa na madaktari uwajani kwenye mchezo wa mwisho wa makundi ya michuano ya Kombe la Dunia wa Agentina dhidi ya Nigeria uliochezwa Jumanne, Uwanja wa Saint Petersburg.

Katika mchezo huo, Argentina waliibuka kidedea na ushindi wa mabao 2-1 na kufuzu kucheza hatua ya 16 bora katika michuano hio ya kombe la dunia nchini Russia.

Maradona alisema ametangaza dau nono kwa mtu yoyote atakayembaini aliyemzushia kuwa amefariki wakati mchezo huo ukiendelea. Alisema alishtushwa na taarifa zilizoanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki kitu ambacho hakikuwa na ukweli wowote.

Soma pia:  Ufaransa, Denmark zafuzu 16 bora Kombe la Dunia

Maradona alipatiwa matibabu wakati mchezo huo unaendelea ambapo hali yake kwa sasa inaendelea vyema.

“Ninamtafuta mtu ambaye alinizushia kuwa mimi nimekufa wakati mchezo unaendelea kitu ambacho sio kweli, yoyote atakayembaini nitamzawadia pauni 8,000,” alisema Maradona

Comments

Comments are closed.

More in Michezo